Deuteronomy 21:1-6

Upatanisho Kuhusu Mauaji

1 aKama mtu akikutwa ameuawa, naye amelala kwenye shamba katika nchi ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa kuimiliki, wala haijulikani ni nani aliyemuua, 2wazee wenu na waamuzi watatoka na kupima umbali kutoka maiti alipolala mpaka kwenye miji ya jirani. 3 bKisha wazee wa ule mji ulio karibu zaidi na yule maiti watamchukua mtamba ambaye hajapata kufanyishwa kazi na ambaye hajafungwa nira, 4na kumpeleka kwenye bonde ambalo halijapata kulimwa au kupandwa mazao na ambapo kuna chemchemi itiririkayo. Huko kwenye hilo bonde, wazee watamvunja yule mtamba shingo. 5 cMakuhani, hao wana wa Lawi, watasogea mbele, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mungu wenu, amewachagua kuhudumu na kutoa baraka katika jina la Bwana, na kuamua mashauri yote ya mabishano na mashambulio. 6 d eNdipo wazee wote wa mji ulio karibu zaidi na huyo maiti watanawa mikono yao juu ya huyo mtamba ambaye shingo yake imevunjwa huko kwenye bonde,
Copyright information for SwhKC